Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli amewaomba wananchi wanaotaka mabadiliko ya kweli na maendeleo ya taifa kuhakikisha wanamchagua yeye kwa kuwa wakimpa nguvu hiyo atatimiza kile wanachotarajia.

Dk. Magufuli ameyasema hayo jana wakati akihutubia umati mkubwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Mbalizi, Mbeya vijijini.

Magufuli ametumia kauli mbiu ya Chadema ‘Peoples Power’ kuwataka wananchi kumpa yeye nguvu hizo.

“Wanasema Peoples power, sasa nipeni hiyo power niwaletee maendeleo,” alisema Magufuli na kusisitiza kuwa  anafahamu watanzania wanahitaji mabadiliko na kwamba mabadiliko hayo hawatayapata popote isipokuwa ndani ya CCM kupitia uongozi wake.

umati wa Magufuli

Aliwataka wananchi kutopotoka kuwa mabadiliko hayawezi kuletwa na chama tawala huku akitoa mfano wa nchi ya China ambayo imeweza kufanya mabadiliko makubwa na kuwa kati ya nchi zinazoongoza kwa uchumi duniani kwa kutumia chama kilekile tawala.

Aidha, Dk. Magufuli alisema kuwa tangu alipotangazwa kuwania urais baadhi ya watendaji mafisadi tayari wameanza kukimbia wenyewe kwa kuwa wanamfahamu vizuri.

“Kama kuna mtendaji ambaye atashindwa kwenda na kasi yangu, atupishe tuwape nafasi hiyo wengine ile wachape kazi za kuwatumika wananchi uskiu na mchana bila kuchoka,” alisema.

Alisema kuwa nia yake kubwa ni kuwafanyia kazi watanzania na sio kitu kingine.

khanga

Magufuli alilazimika kusimama mara kadhaa njiani baada ya wananchi kumtaka japo awasalimie.

 

Lowassa, Magufuli Uso Kwa Uso Kwenye Mdahalo
"Dk. Slaa Kujiunga Na Uzinduzi Wa Ukawa Jangwani"