Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Aprli 29, 2020, imeamuru kukamatwa kwa Mbunge na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kwa kukiuka Masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Hayo yamejiri baada ya Kiongozi huyo kushindwa kufika Mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri lake.

Imeelezwa kuwa hata wadhamini wa mshtakiwa huyo (Zitto Kabwe) hawakufika Mahakamani hapo kueleza yanayomsibu mshtakiwa.

Tanzia: Mbunge Ndasa afariki dunia, Ndugai ahairisha vikao vya Bunge

Hatahivyo Mahakama imepanga Mei 29, 2020 kutoa hukumu ya kesi hiyo ya uchochezi ambapo Zitto anatuhumiwa kulihusisha Jeshi la Polisi katika mauaji ya watu zaidi ya 100 mkoani Kigoma.

Corona: Hospitali ya Nairobi kupima sampuli 900 kwa siku, kupima ni Sh 200,000
Mh. Mwakyembe usiingie kwenye mtego huu