Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Mbinga wahakikishe kuwa wanaunda kanda za kilimo na kuwasambaza maafisa kilimo wao badala ya kuwaacha wakae maofisini.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

“Mkurugenzi wa TC na DC chuja maafisa kilimo ulionao na uhakikishe wanabakia watatu tu. abaki DALDO, mtu wa horticulture na mthamini, wengine wote wasambaze kwenye kanda ili wasimamie wakulima wakiwa huko huko. Hili litekelezwe na Mkuu wa Wilaya ulisimamie,” amesema Majaliwa

Aidha, amewataka maafisa kilimo wa zao la kahawa waende vijijini na kufanya sensa ili waweze kubaini wana wakulima wangapi wanaozalisha kahawa.ili wapate idadi ya miche ambayo itakuwa inagawiwa kwa wakulima hao.

Hata hivyo, Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka maafisa ushirika wa wilaya hiyo wakasimamie uundwaji wa AMCOS mpya na kuimarisha zile za zamani ambazo zinafanya kazi vizuri.

 

Makonda ajitolea kujenga nyumba ya mwandishi
Watu wasiojulikana wazidi kutikisa