Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha, Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha, Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.  

Waziri Mkuu alichukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya ukaguzi maalum uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019, lengo la ukaguzi huo ikiwa ni kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo katika kikao chake na waziri na naibu wa waziri wa Ujenzi na uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menajiment ya TPA, Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI).

Katika taarifa iliyotolewa na kwa umma Majaliwa, amemuagiza pia CAG kufanya ukaguzi maalumu katika bandari ya Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Aidha amesema kuwa miongoni mwa mambo yanayoikosesha serikali ni pamoja na msamaha wa kodi wa shilingi billioni 2 iliyoutoa kwa cha saruji cha Mbeya licha ya kukataliwa na kamati ya msamaha.

Aidha amesema kuwa TPA iliidhinisha malipo ya billioni 8.2 kwenda bandari ya Kigoma kwaajili ya kufanya malipo mbalimbali huku ukomo wa bandari hiyo ni billioni 7.4

“Fedha hizo zilitumika kufanya malipo yasiyostahili akiwemo mfanyabiashara wa duka la ujenzi mjini Kigoma Eliya Mtinyako aliyelipwa zaidi ya Sh900milioni, hakuna nyaraka zinazoonesha alilipwa kwa sababu zipi na hakuwahi kutoa huduma yoyote na wala si mzabuni. Pia amelipwa bila nyaraka za madai.” amesema Majaliwa.

Onyo kwa vyuo binafsi vya Famasi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 28, 2020