Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Samia Suluhu Hassan imekanusha taarifa zilizokuwa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusika wake kwenye VICOBA, SACCOS na vikundi vingine vya kukopeshana.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu wa Makamu wa Rais, Waziri Rajab Salum imeeleza kuwa watu wanaosambaza habari hizo ni matapeli.

“Tunatoa wito wa kuwapuuza watu wa namna hiyo huku vyombo vyetu vikiwasaka ili kuwajua na taratibu za kisheria kufuatwa dhidi yao,” imeeleza taarifa hiyo.

Katibu huyo wa Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kuwafichua watu hao kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya husika ili kuzuia wizi kwenye mitandao.

Habari

Magufuli: Bado kuna nafasi ya Kutafuta maridhiano Zanzibar
Mwenyekiti wa Majaji Wastaafu amtetea Rais Magufuli katika hili