Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajia kuruzu nchini Tanzania baada ya kuanza ziara ya wiki moja barani Afrika, huku Maafisa waandamizi wa Marekani wakisema atajadili ushiriki wa China katika masuala ya teknolojia na uchumi barani Afrika, ambayo yanalitia wasiwasi Taifa hilo. na nafasi ya China katika urekebishaji wa madeni kwa nchi za Afrika.
Mojawapo ya nchi tatu ambazo Harris atazuru ni Zambia, ambayo ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutolipa deni lake kuu wakati wa janga la UVIKO-19, na inafanya kazi na wakopeshaji wake, pamoja na China, kufikia makubaliano.
Harris ambaye amekuwa nchini Ghana tangu Machi 26, 2023 anatarajia kuwasili nchini Tanzania kati ya Machi 28 – 31, 2023, kabla ya kuelekea kituo chake cha mwisho ambacho ni Zambia, atakapokuwa kwa siku mbili za Machi 28 – April Mosi, 2023.
Akiwa nchini Ghana, Kamala Harris alimsifu Rais wa Taifa hilo Nana Akufo-Addo kwa kanuni zake za kidemokrasia, wakati wa ziara yake na kiongozi huyo wa Afrika Magharibi, ambaye anakabiliwa na tatizo la kumaliza mfumuko wa bei na wasiwasi mpya kuhusu usalama wa kikanda.
Siku ya Jumatatu, alikaribishwa katika ikulu ya rais wa Ghana ya Jubilee House, ambapo aliahidi usaidizi wa usalama katika taifa hilo, na kuongeza uwekezaji huko, akitangaza msaada wa dola milioni 100 kwa eneo hilo.
Hata hivyo, Akufo-Addo alisimamia moja ya uchumi unaokua kwa kasi duniani kabla ya janga la COVID-19. Hata hivyo, gharama ya chakula na mahitaji mengine imekuwa ikipanda kwa kasi, na nchi hiyo inakabiliwa na mzozo wa madeni huku ikihangaika kufanya malipo.