Jeshi la polisi la Uingereza limetangaza hali ya tahadhari kwa makanisa 47,000 nchini humo baada ya jana vijana wawili wenye umri wa mika 18 kuvamia kanisa na kumuua kikatili kwa kumchinja padri wa Kanisa Katoliki, Kaskazini mwa Ufaransa.

Tahadhari hiyo imeambatana ulinzi mkali katika kila kanisa chini Uingereza kutokana na tukio la mauji ya padri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 84 nchini Ufaransa kuwa la kwanza kufanywa na kundi linalojiita Islamic State (IS) ndani ya kanisa katika nchi za Magharibi.

“Kufuatia matukio ya Ufaransa, tunasisitiza ushauri wetu na kuelekeza ulinzi kwenye maeneo yote yenye makanisa na sehemu za ibada. Na leo tumetoa ushauri muhimu kwa kupitia upya ulinzi wao na kuchukua tahadhari zaidi,” Kamishna msanidizi wa Polisi, Nel Basu alisemea.

Watekelezaji wa mauaji hayo ya kikatili walivamia kanisani muda wa ibada huku wakiwashikilia kwa muda waumini wa kanisa hilo. Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwaua vijana hao wadogo.

Uchunguzi wa Polisi umeonesha kuwa mmoja kati ya watekelezaji wa tukio hilo, Adel Kermiche alijirekodi kipande cha video kwenye simu yake mwezi mmoja uliopita na akamtumia rafiki yake akisema “nitatekeleza ndani ya kanisa”.

 

Video: Makonda Atoa Ujumbe Muhimu Kwa Wakazi Wa Dar
Padri auawa akiendesha ibada kanisani