Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, leo  amezindua ujenzi wa barabara ya shimo la udongo iliyopo kurasini,wilaya ya Temeke inayojengwa kwa kiwango cha zege, amesema kuwa Dar es Salaam inajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kila mmoja ana  mchango wa kusaidia kadri awezavyo kama walivyojitokeza wazawa wa Kampuni ya Grand Tech kujenga barabara hiyo.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja huku akiongeza kuwa wazawa hao ndiyo wakwanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kujenga barabara na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili waendelee kusaidia katika maeneo mengine.

Aidha, Makonda amesema kuwa barabara hiyo inatija kubwa kwa Serikali kwani ujenzi wake kwa kiwango cha zege utasaidia malori kupita bila kufanya uharibifu kama ilivyokuwa awali, na kuongeza kuwa ujenzi huo unatarajia kukamilika ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Grand Tech, Patrick Mwakitwange, amesema kuwa wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali kwani eneo hilo la shimo la udongo lilitengwa kwaajiri ya shughuli za bandari hivyo ujenzi huo utarahisisha shughuli hizo na kuunga mkono  jitihada za Rais Magufuli.

.

Video: Kijana aliyeishi maisha ya ajabu, asimulia mazito
Serikali yazindua mpango kazi kupinga ukatili kwa wanawake na watoto