Kiungo kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima, amesema Young Africans imemfanyia kitu kikubwa tangu alipojiunga nayo hadi alipoagwa jana Alhamis (Julai 15).

Niyonzima aliagwa kwa heshima mbele ya Mashabiki waliojitokeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu FC, ambao ulimalizika kwa Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kiungo huyo alimesema katika kipindi chote akiwa Young Africans, ameishi kwa amani akiwa ndaninya timu na akiwa na familia yake hapa nchini.

“Naweza kusema Young Africans ni familia yangu, nimeishi Tanzania mimi na familia yangu kwa amani, wana Yanga walinipokea kwa upendo mkubwa sana sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaambia asante.”

“Young Africans nimeichezea kwa mapenzi makubwa japo niliitajika na timu nyingi ila niliichagua klabu hii. Nawashukuru Wachezaji wenzangu, Viongozi, Mashabiki na GSM pamoja na watu wote waliofanikisha mimi kuwa hapa, nawapenda sana na nchi yangu ya Rwanda wanaipenda klabu ya Young Africans” alisema Niyonzima.

Ifahamu kwa undani historia ya mradi wa bandari ya Bagamoyo
Bocco, Gomes wasambaza Ligi Kuu