Rais wa Marekani Joe Biden ameweka wazi kwamba hataondosha vikwazo dhidi ya Iran hadi pale Taifa hilo litakapoheshimu makubaliano yaliyofikiwa katika mkataba wa nyuklia, licha ya kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei kuhimiza Marekani kuviondoa vikwazo.

Mkataba baina ya Iran na mataifa yaliyo na nguvu duniani ulifikiwa mwaka 2015, lakini uliingia dosari baada ya Rais aliyemaliza muda wake Donald Trump kujiondoa mwaka 2018 na kisha kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo.

Januari 4, Iran ilitangaza urutubishaji wa madini ya Urani kwa hadi asilimia 20 juu ya kiwango kilichokubalika katika mkataba huo.

Biden ameahidi kuirejesha Marekani katika mkataba wa nyuklia lakini hadi pale Iran itakapofuata makubaliano.

Iran imetishia kuwazuia wakaguzi wa kimataifa kwenye vinu vyake vya nyuklia ifikapo Februari 21 ikiwa vikwazo vya Marekani havitaondolewa.

Kichapo cha Namungo FC chamuibua Masau Bwire
Ebola yaibuka tena Congo