Ndege ya shirika la American Airlines, iliahirisha safari ya kuelekea Dallas baada ya wanaume wawili walio vaa mavazi yenye asili ya kiarabu kuagana kwa kupungiana mikono.

Uongozi wa shirika hilo umesema kuwa ulichukua uamuzi huo kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa wafanyakazi wa ndegehiyo na abiria kuwatilia shaka  wanaume hao.

Kwa upande wa wanaume hao, Isam Abdallah, na  Abderraooof Alkhawaldeh, wameomba uchunguzi huru ufanyike kwa kubaguliwa kwao.

Abdallah amesema kuwa mhudumu wa ndege hakuwa huru kuanza safari, baada ya yeye na abilia mwenzie kuingia kukaa na kuagana ndani ya ndege hiyo.

Alkhawaldeh, yeye amesema kuwa ni msafiri wa ndege wa mara kwa mara tangu mwaka 1989 na haoni sababu ya kutiliwa shaka.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 22, 2019
Mbaroni kwa kukutwa na nyama ya wanyama pori