Mashabiki wa klabu ya Liverpool wameonyesha kuchukizwa na mwenendo wa meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers, kwa kumshambulia kwa maneno makali kupitia mitandao ya kijamii.

Rodgers, alikua na wakati mgumu wa kubaini ni vipi asivyotakiwa katika kipindi hiki huko Anfield, baada ya kikosi chake kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa Europa League dhidi ya FC Sion ya nchini Uswiz.

Kwa nyakati tofauti mashabiki wa The Reds, walianza kuandika ujumbe mzito kupitia mitandao ya kijamii mara baada ya mchezo huo kumalizika ambapo mmoja kati yao aliandika “Kama Rodgers anaheshimu historia ya klabu ya Liverpool, anapaswa kufungasha na kuondoka”.

Mwingine alidiriki kuandika ujumbe wa kumpa muda meneja huyo kutoka Ireland ya kaskazini kwa kumwambia mchezo dhidi ya Everton utakua wa mwisho kwake mwishoni mwa juma hili, ni bora akautumia muda huu kuagana na anaowafahamu mjini Liverpool.

Rodgers, amekua na wakati mgumu tangu alipoajiriwa klabuni hapo mwaka 2012, licha ya kujitahidi kuonyesha dhamira ya kufanya vyema lakini amekua akiambulia patupu na kujikuta hana ubingwa wa michuano yoyote tofauti na mameneja waliomtangulia klabuni hapo.

Matokeo ya sare ya kufunga bao moja kwa moja dhidi yab FC Sion yanaendelea kuipa wakati mgumu klabu hiyo kwenye msimamo wa kundi B la michuano ya Europa league, kutokana na matokeo kama hayo kupatikana katika mchezo wa kwanza ulioshuhudia wakipambana dhidi ya Bordeaux ya nchini Ufaransa.

Katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini England msimu wa 2015-16, Liverpool wameshapoteza michezo miwili miongoni mwa michezo saba waliyocheza mpaka sasa huku wakitoka sare mara mbili na kushinda michezo mitatu, hali inayowafanya wakae katika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

 

Mgombea Ubunge Atekwa, Watekaji Watoa Masharti
Gareth Bale Aitwa Kikosini Wales