Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba SC Barbara Gonzalez ametangaza viingilio vya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club utakaochezwa siku ya Jumamosi (April 03) mzunguko ni 10,000 zitauzwa tiketi 8000 VIP B 25,000 na VIP A 40,000.

Barbara ametangazaviingiliohivyo leomchana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, baada ya Shirikisho la soka nchini TFF kuthibitisha taarifa kutoka CAF ya kuruhusiwa kwa mashabiki 10,000 kuingia Uwanjani kushuhudia mchezo huo wa Jumamosi.

Barbara amesema shabiki ambaye hatakuwa na barakoa hataruhusiwa kuingia uwanjani siku ya Jumamosi na kila mtu anapaswa kukaa umbali wa siti 3 na mwenzake pia mauzo ya tiketi uwanjani hayataruhusiwa hivyo kila shabiki anunue tiketi yake mapema.

Naye mkuu wa idara ya habari na mawasilinoHaji Sunay Manara amesema: “Kwa mashabiki wetu watu 10,000 ni watu wachache sana. Hatutarajii siku ya mchezo watu wawe bado hawajanunua tiketi sababu siku ya mchezo CAF hawaruhusu tiketi kuuzwa uwanjani.”

“Hakuna namna lazima tupate ushindi kwenye mchezo huu. Hii itakuwa ni DO OR DIE; SEASON TWO na hiyo ndio itakuwa kauli mbiu yetu.”

“Kikosi chetu kipo vizuri wachezaji wengine wameshawasili na wengine wanaendelea kuwasili. Afya za wachezaji zipo vizuri tofauti na zinavyoandikwa baadhi ya sehemu na tutaendelea kuchukua hatua.”- Manara.

Tayari AS Vita wameshaanza safari ya kuja nchini kwa ajili ya mchezo huo, ambao umepangwa kuchezwa mishale ya saa kumi jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi A kwa kufikisha alama 10, ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama 7, AS Vita inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 4 na AlMerrikh wanaburuza mkia kwa kupata alama moja kwenye michezo minne waliocheza.

Sarpong: Ninapenda kufunga
Namungo FC: Jumapili tuna jambo letu