Mshambuliaji wa Klabu ya Young Africans, Michael Sarpong amesema kitu ambacho anakipenda kukifanya akiwa uwanjani ni kufunga mabao kwa ajili ya timu yake.

Young Afrcans ikiwa imetupia jumla ya mabao 36  kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 23 amehusika katika mabao matano ambapo amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.

Sarpong amesema: “Nikiwa uwanjani ninapenda kufunga na kuipa ushindi timu yangu hakuna jambo jingine ambalo huwa ninapenda. Ikitokea nikashindwa basi nitatengeneza nafasi kwa mwenzangu.

“Ukweli ni kwamba mashabiki wanapenda kuona timu ikishinda hilo ninalijua hata mwalimu pia amekuwa akituambia suala hilo, imani yangu nitafanya hivyo katika mechi zetu zijazo,”

Wakati huo huo Kaimu Kocha Mkuu wa Young Africans, Juma Mwambusi amesema kuwa maendeleo ya nyota wake ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Mapinduzi Balama, Dickson Job yamezidi kuimarika.

Mwambusi amesema: “Kila mchezaji anaonekana kuwa na furaha na taratibu wale ambao hawakuwa fiti wanarudi, Mapinduzi Balama amepewa program maalum huku wachezaji wengine wakiwa wameanza mazoezi.

“Fiston naye kwa sasa anaendelea vizuri ni jambo jema kwetu na tunaamini wale wengine ambao hawajawa kwenye ubora wataimarika.”

Cavani kubaki Man Utd
Masharti kwa mashabiki watakaokwenda kwa 'Mkapa'