Kikosi cha Namungo kinaendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo wa mzunguuko watatu wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi dhidi ya Nkana FC ya Zambia utaochezwa Jumapili (April 04), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa Namungo, Kindamba Namlia amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani kwa mara ya kwanza tangu walipotinga hatua ya Makundi.

Kindamba amesema wachezaji wote wa Namungo FC wapo kwenye ari kubwa ya kujiandaa kuelekea kwenye mchezo huo chini ya ukufunzi wa kocha wao kutoka Zanzibar Hemed Morocco.

“Kikosi chetu kinaendelea vizuri na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ijumaa dhidi ya wageni wetu Nkana kutokea Zambia.” Amesema kindamba

 “Mpaka sasa tumekamilisha asilimia kubwa ya maandalizi ya mchezo huo na tunasubiri muda wa mchezo ufike, kikosi chetu kiko kamili kwani idadi kubwa ya majeruhi tayari wamepona na wanaendelea na mazoezi japo tutaendelea kukosa huduma ya mshambuliaji wetu Bigirimana Blaise ambaye amekuwa na majeraha ya muda mrefu.”

Namungo FC tayari imeshacheza michezo miwili ya hatua yamakundi Kombe la Shirikisho dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco nakukubali kufungwa 1-0, kicha wakafungwa 2-0 dhidi ya Pyramid ya Misri.

Masharti kwa mashabiki watakaokwenda kwa 'Mkapa'
Miquissone, Kagere kutinga kambini leo