Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaujulisha Umma kuwa, Mei 23, 2021, majira ya saa 8 mchana katika Bandari ya Dar es Salaam, Mashine ya kunyanyua vitu vizito (Crane) iliyokuwa ikishushwa
kutoka kwenye Meli ya LCT AJE 1 ilipata ajali ya kutumbukia Baharini.

Mashine hiyo yenye uzito wa takribani tani 70, iliwasili kwa Meli katika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea Visiwa vya Songongo na ilikuwa ikishushwa katika eneo la Gati ya Malindi.

Kupitia taarifa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawatoa hofu Wananchi na Wateja wote kuhusiana na tukio hili na kwamba zoezi la kuipoa Mashine hiyo linaendelea.

Taarifa zaidi kuhusu zoezi la uopoaji zitatolewa katika vyombo vya habari, tovuti pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii za TPA.

Morocco: Nguvu nazipeleka ligi kuu
Rais Mwinyi afanya Uteuzi Zanzibar