Vyombo vya dola nchini Saudi Arabia, vinamshikilia mfanyakazi mmoja wa hotel ya kigeni kwa kosa la kuweka mtandaoni kipande cha video inayomuonesha akiwa analishwa chakula na mwanamke.

Mwanamke anayeonekana kwenye video hiyo akimlisha kijana huyo, amevalia mavazi rasmi ya baibui na kujifunika sura yake kama ilivyo kwa utamaduni wa nchi hiyo, lakini kitendo cha kumlisha mwanaume hadharani kimetajwa kuwa kinakashfu tamaduni na desturi ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya kazi Jumapili hii, imeeleza kulaani kitendo hicho na kuweka wazi kuwa mhusika atachukuliwa hatua kali za kisheria. Mwanamke aliye kwenye video hiyo ambaye pia ametajwa kuwa mfanyakazi wa hotel hiyo anahojiwa, kwa mujibu wa wizara hiyo.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mtuhumiwa huyo ni raia wa Misri.

Mwendesha mashtaka wa serikali pia ametoa tamko lake na kuwataka watu wote wanaoingia nchini humo kuhakikisha wanaheshimu tamaduni za jamii ya Saudi.

 

Harry Kane kuwa shuhuda England Vs Uswiz
Ajali mbaya yaua wanne Kilimanjaro, Rombo