Star wa filamu na vichekesho nchini Marekani amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa mgongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Malibu hills.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 alipata ajali hiyo akiwa na gari yake aina ya Plymouth Barracuda huku ndani ya gari hilo kukiwa na watu watatu lakini mmoja hakupata tatizo lolote japokuwa gari iliharibika vibaya.

Mke wa msanii huyo Enika Hart amethibitisha mume wake huyo kufanyiwa upasuaji wa sehemu ya mgongo na sasa anaendelea vizuri.

‘Tunashukuru kevin anaendelea vizuri kwasasa aalifafanikiwa kufanyiwa upasuaji sehemu ya mgongo na hali yake kwa sasa imeanza kukaa sawa, tunashukuru kwa maombi na salamu mbalimbali za pole kupitia mitandao ya kijamii’ alisema Eniko.

Mtandao wa tmz ulirpoti kuwa Hart alikuwa akiendeshwa, ghafla dereva wake alishindwa kulimudu gari hilo na kuparamia kingo za barabara ya mji huo.

Hata hivyo polisi wa mji huo walithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kwamba Hurt alikuwa ameumia maeneo ya mgongoni na kufanyiwa huduma ya kwanza nyumbani kwake kwa matibabu ya awali na baadae kupelekwa hospitali.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 8, 2019
Harmonize, Babu Seya wafunga ndoa za kimyakimya