Robert Rhameek aka Meek Mill ameamua kukinusha kupitia twitter kwa kumchana Drake kuwa ni ‘fake’ na haandiki mashairi yake mwenyewe hivyo asifananishwe nae.

Rapper huyo wa MMG ambaye album yake mpya ya ‘Dreams Worth More Than Money’ inaonekana kufanya vizuri, ametumia maneno machafu katika tweets kadhaa akimchana Drake kuwa na uwezo hafifu wa kuandika na kurap. Anadai hiyo ni sababu inayomfanya Drake asiandike chochote kuhusu album ya Meek Mill kwenye mtandao.

“Stop comparing drake to me too…. He don’t write his own raps! That’s why he ain’t tweet my album because we found out!” Meek Mill ametweet mapema leo asubuhi.

Katika tweet nyingine, Meek ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na Nicki Minaj, amemkejeli Drake ambaye aliwahi kuripotiwa kuwa uhusiano na Nicki, kwa kupost picha ya Drake akiwa na Nicki kwenye video ya wimbo wa ‘Anaconda’.

Rapper huyo mzawa wa Philadelphia pia alijigamba kuwa uhusiano wake na Nicki Minaji wala mtu yeyote hakujachangia mafanikio yake kama wengi wanavyodai.

Ni kama Meek ameamka na akili zake za usiku kwa kuwa amewazungumzia rappers wengine wengi kwenye tweet zake akiwemo J Cole, Lil Wayne, Jay Z, Rick Ross na wengine kwa namna tofauti tofauti.

Said Kubenea Ajitosa Kuwania Ubunge Wa Ubungo
Lembeli Aeleza Kilichomuondoa CCM Kuhamia Chadema