Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameishauri serikali kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundisha masomo ya shule za msingi, sekondari na vyuo ili kuwawezesha wanafunzi kupata uelewa.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizindua mashindano ya ya mashairi ya Meya wa jiji yaliyodhaminiwa na kampuni ya mabati ya Alaf.

Amesema kuwa ni vyema kama nchi kuthamini lugha ambayo ndiyo inayounganisha Watanzania wote na si kuiga lugha za nchi nyingine.

“Ukienda Uganda wanazungumza lugha yao na wakenya pia hutumia lugha zao lakini sisi Watanzania tunapenda kuiga lugha za wenzetu na kuacha kupenda vyetu,” amesema Mwita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili katika chuo kikuuu cha Dar es Salaam Dkt. Elnester Mosha amempongeza Mwita kwa kuanzisha mashindano hayo kwa kuwa yanasaidia kukuza Kiswahili nchini.

Video: Lissu atuma waraka mzito kwa Magufuli, Makontena 10 ya Makonda yazua utata mpya mnadani
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 2, 2018