Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF), umepangwa kufanyika ifikapo Oktoba 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Najaha Bakari amesema fomu kwa ajili ya wadau wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali zilianza kutolewa jana na mwisho wa zoezi hilo ni Oktoba 24, mwaka huu.

Najaha amezitaja nafasi zinazowaniwa ni pamoja na Rais, Makamu Rais, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina na nafasi tatu za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

“Ada ya fomu kwa nafasi tano za juu ni Sh. 100,000 na kwa nafasi ya ujumbe ni Sh. 50,000. Usaili wa wagombea utafanyika siku mbili kabla ya uchaguzi,” amesema Najaha.

Ameongeza, kwa kuwataka wadau wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi za uongozi ili chama hicho kipate safu ya viongozi iliyokamilika kwa maendeleo ya mchezo huo.

Hassan Mwakinyo amfuata Liam Smith
Ibenge aihofia Young Africans Ligi ya Mabingwa Afrika