Shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwengiuni WHO, limezindua ripoti mpya inayowataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs, ambayo hukatili Maisha ya watu milioni 17 kila mwaka.

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ripoti hiyo ni kumbusho la tishio linaloletwa na NDCs na hatari zake na kwamba zipo hatua ambazo ni za gharama nafuu ambazo kila nchi bila kujali kiwango chake cha kipato kote duniani, inapaswa kuzichukua na kufaidika nazo ili kuokoa maisha ya watu na gharama.

Namshukuru Rais Afuko-Addo , Waziri mkuu Store na Michael Bloomberg kwa uongozi wao na maono katika kushughulikia changamoto za kimataifa za afya na ili kusongesha mchato wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama moyo, kisukari, saratani, mfumo wa hewa na mengineyo, WHO imemteua tena kwa miaka mingine miwili, Michael Bloomberg ukiwa ni muhula wake wa tatu.

Wahudumu wa afya wakimpatia matibabu mmoja wa wagonjwa wenye uhitaji wa huduma. Picha na UN.

Akikubali jukumu hilo, Bloomberg amesema” Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari, matatizo ya mapafu na saratani huuwa kimyakimya lakini yanaweza kuzuilika kwa ushirikiano, nipo tayari kuendelea kuchagiza uwekezaji wa kuokoa maisha kwa NCDs na kufanyakazi bega kwa bega na Dkt. Tedros.”

Hata hivyo, WHO imesisitiza kwamba, bado kuna uelewa hafifu kwa umma kuhusu uhusiano uliopo baina ya NCDs na hatari ya vichocheo vyake kama matumizi ya tumbaku na pombe, lishe duni na kutofanya mazoezi hivyo limezitaka nchi kuongeza juhudi katika upande huo na kuhimiza suala la kujali afya.

Shirika hilo la afya Ulimwenguni, linasema lengo kubwa ya ripoti ya sasa na wito wake ni kuhakikisha hatua zitakazochukuliwa zinaokoa Maisha ya watu milioni 50 ifikapo mwaka 2030 kote duniani.

Ruto atoa wito msamaha wa madeni WB na IMF
Mvua yazidi kunyesha mafuriko yakiuwa 300