Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nchi zenye maendeleo duni – LDC5, umeungana na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kuadhimisha mafanikio ya wanawake na wasichana Duniani.
Katika Mkutano huo, wito wa uwezeshaji umesisitizwa na ulitawala sehemu kubwa ya mjadala katika Kituo kikuu hicho cha mikutano, huku Wanawake Vijana, Wanasayansi na Wavumbuzi, kama Timu ya Roboti ya Wasichana wa Afghanistan, wakihimiza kauli mbiu ya “Usikate tamaa!”
Fatima, Katibu Mkuu wa Mkutano huo, Rabab wa LDC5 amesema, “leo inapaswa kuwa siku ya kutafakari na kudhamiria kufanya vizuri zaidi, lakini pia iwe sherehe, kusherehekea mchango wa kimsingi unaotolewa na wanawake na wasichana, mara nyingi dhidi ya vikwazo, kwa mafanikio ya ulimwengu bora.”
LDC5, imefanya maadhimisho karibu na Maman, ambayo ni sanamu ya shaba na chuma cha pua ya msanii Louise Bourgeois, ambayo inayoonekana katika ukumbi mkuu wa Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Qatar.