Baada ya kuhangaika kujisafisha kufuatia kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni, mwanaridha kutoka nchini Uingereza, Mohamed “Mo” Farah, amethibitisha kushiriki mashindano ya London Anniversary Games.

Farah ambaye aliibuka kidedea katika mbio za mita 5000 na 10,000 wakati wa michuano ya Olympic ya mwaka 2012, amethibitisha kushiriki michuano hiyo ambayo ana imani itamsaidia katika maandalizi yake kuelekea mpambano wa dunia ambao umepangwa kufanyika mjini Beijing, China mwezi Ogosti.

Mwanariadha huyo mzaliwa wa Somalia, amesema ni jukumu lake kushiriki michuano hiyo ambayo itafanyika jijini London Julai 24 kwenye uwanja wa Olympic kutokana na uhitaji wa kuwa na maandalizi ya kutosha katika kipindi hiki.

Farah amesema kutokana na dhamira yake, anaamini sio muda tena kwa mashabiki kuendelea kujadili sakata lililokua likimkabili la matumizi ya dawa za kusisimua misuli ambalo alijitahidi kulipinga na kufanikiwa kwa asilimia 100.

Farah, mwenye umri wa miaka 32, alilazimika kujiondoa kwenye michuano ya ‘Diamond League’ iliyofanyika mjini Birmingham, kufuatia sakata hilo ambalo lilimuhusisha kocha wake Alberto Salazar, hatua ambayo anaamini ilimpotezea sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya dunia.

Rais Wa FC Barcelona Auchekesha Umma Na Hadhithi Ya Sungura
Serena Aendelea 'Kuchachafya' Jijini London