Kiungo kutoka nchini Ureno Joao Moutinho amefichua siri iliyodumu kwa miaka minne moyoni mwake kwa kusema alikaribia kujiunga na klabu ya Tottenham mwaka 2012.

Spurs waliwahi kukubali kutoa kiasi cha Pauni milioni 24, kwa ajili ya kumsajili Moutinho alipokua akiitumikia FC Porto ya nchini kwao Ureno, lakini changamoto ya kupatikana kwa vibali vya kufanyia kazi nchini England vilikwamisha mpango huo.

Mwaka mmoja baadae Moutinho alijiunga na klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa, na leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Spurs katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

“Ni kweli, nilikaribia kujiunga na Spurs miaka minne iliyopita,” Alisema Moutinho alipokua katika mkutano na waandishi wa habari.

“Kwa sasa nipo AS Monaco na inanilazimu kufikiria namna ya kuisaidia klabu hii, kwani yaliyopita yameshapita na hayana maana kuwa sehemu ya kichwa changu katika kipindi hiki.

Msimu uliopita Tottenham iliifunga AS Monaco mabao 4-1 katika michuano ya Europa League, lakini Moutinho anaamini jambo hilo lilitokea kwa bahati mbaya na ameahidi makosa waliyoyafanya yatafutwa katika mtanange wa hii leo.

“Kila timu imekua na mabadiliko makubwa tangu tulipokutana msimu uliopita, lakini ninaamini AS Monaco imeimarika zaidi na hatuna budi kudhirisha jambo hilo tutakapokua uwanjani.

“Spurs watahitaji kuendeleza wimbi la ushindi dhidi yetu, lakini hatutokubaliana na jambo hilo mpaka tuhakikishe tumelipiza kisasi cha kufungwa msimu uliopita. Alisisitiza Moutinho.

AS Monaco na Spurs zimepangwa katika kundi E kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya sambamba na Bayer Leverkusen na CSKA Moscow.

Wagner Ribeiro: Neymar Amekataa Mshahara Wa Pauni 650,000
Barack Obama ni kati ya watoto waliolelewa na mzazi mmoja, nini chanzo cha malezo hayo?