Kenya, mwendesha bodaboda mmoja anayejulikana kwa jina la Samuel Njeru anashikiliwa na polisi kwa kosa la jinai la kuchoma moto nyumba waliokuwa wakiishi wazazi wake.

Samuel aliamua kufanya tukio hilo mara baada ya wazazi wake kumkataa mwanamke aliyepanga kumuoa.

Njeru alirudi nyumbani usiku akiwa amelewa pombe na kuanzisha ugomvi na wazazi wake kuhusu mwanamke anayetaka kumuoa.

Baada ya ugomvi huo Njeru aliamua kuwasha moto na kuteketeza nyumba wanayoishi wazazi wake.

Hivyo majirani walisaidia kuuzima moto kwani ulikuwa uteketeze nyumbe yote.

Aidha Kiongozi wa Polisi amewataka wazazi wake  kumaliza mgogoro huo na kijana wao.

Hassan Banyai ainawa Njombe Mji FC
Ukimwi wazidi kuwa tishio nchini