Beki wa kulia wa Arsenal Mathieu Debuchy anahofiwa kuumia baada ya kuchezeshwa kwa mara ya kwanza katika michezo ya ligi ya nchini England kwa msimu huu hapo jana.

Mwenye wa Arsenal Arsene Wenger, aliwaambia waandishi wa habari kuhusu hofu iliyotanda dhidi ya beki huyo kutoka nchini Ufaransa, ambaye alilazimika kutolewa nje ya uwanja katika dakika ya 16 ya mchezo dhidi ya Bournemouth ambao walikubali kichapo cha mabao matatu kwa moja.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, anahofiwa kuumia nyama za paja lakini bado haijathibitishwa ni kwa kiasi gani.

“Nimezungumza na watu wa tiba, lakini wamenihakikishia baada ya saa 48 tutakua tumeshapata majibu halisi,”

“Ninahofia atakua ameumia, lakini siwezi kuelezea ni kwa kiasi gani, ila ameonekana ameumia.” Alisema Wenger.

Katika mchezo huo mabao mawili ya Arsenal yalifungwa na mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez, na lingine moja likazamishwa wavuni na Theo Walcott, huku Callum Wilson akifunga bao la kufutia machozi kwa AFC Bournemouth.

Debuchy amekua na bahati mbaya ya kuumia mara kwa mara tangu alipojiunga na Arsenal akitokea Newcastle Utd mwaka 2014.

Wilhelm Gidabuday Katibu Mkuu RT
Makonda awanyooshea kidole watumishi aliodai wanaotumia ‘hirizi’