Tume ya uchaguzi ya Taifa (NEC) imejibu taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao kuwa imekuwa ikitumia wanajeshi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo wa BVR pamoja na shughuli nyingine.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Kailima Kombwey amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa tume hiyo ina wataalam wa kutosha wa mifumo ya TEHAMA ambao wanawatumia katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

“Katika kipindi kama hiki, huwa tunatafuta vijana waliomaliza vyuo vikuu kwa ajili ya kusaidia kazi mbalimbali kama ya kuandikisha wapiga kura kwa njia ya BVR. Tumeajiri vijana zaidi ya 600 kutoka katika vyuo vikuu hadi vya kati,” alisema Bw. Kombwey.

Katika hatua nyingine, juzi tume hiyo ilikanusha taarifa kuwa namba iliyotolewa kwa ajili ya kuhakiki taarifa za mpiga kura kwa njia ya simu ni mipango ya kuhujumu ili kuharibu nafasi yao ya kupiga kura Oktoba mwaka huu. Tume hiyo ilifafanua kuwa utaratibu huo ni salama na umewekwa kwa lengo la kuokoa muda.

Kikosi Cha U13 Chatangazwa
Saanya Akabidhiwa Jukumu Zito Jumamosi