Baraza la mitihani la taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya darasa la saba 2019 na kueleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 81.50 ya watahiniwa ambao walikuwa 933,369.

Mwanafunzi aliyetangazwa kuongoza kitaifa ni Grace Manga kutoka shule ya msingi Graiyaki ya mkoani Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka shule ya msingi Paradise ya Geita na nafasi ya tatu ni Loi Kitundu kutoka shule ya msingi Mbezi ya Dar es salaam.

Katibu mtendaji wa NECTA, Dkt. Charles Msonde amesema watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwasababu mbalimbali ikiwemo kufanya udanganyifu, ambapo baraza limesema limebaini walimu wakuu, wasimamizi na walinzi walihusika kwenye udanganyifu.

Dkt. Msonde ameeleza kuwa katika kikao walicho kaa leo, tayari wamesha zitaarifu mamlaka za ajira na sheria ili ziwachukulie sheria na hatua wahusika.

Miaka minne ya kifo cha Filikunjombe, ibada maalumu yafanyika Ludewa
Mwakinyo atamba kumchakaza Mfilipino