Rapa wa Young Money, Nicki Minaj amejikuta katikati ya mahakama ya mashabiki wa Instagram baada ya kupost picha yenye utata wa ubakaji wakati wa sherehe za ‘Halloween’.

Mkali huyo wa ‘Anaconda’ ali-screen shot picha iliyowekwa na DJ Clue na kuipost kwenye akaunti yake ikionesha taswira ya ‘Bill Cosby’ katika muonekano wa ‘Halloween’ akiwa amemshikilia ambaye anaonekana hajitambui, lakini anamuwekea dawa za kulevya kwenye kinywaji chake.

Bill Cosby

Kitendo hicho kilitafsiriwa na wengi kama udhalilishaji na uhamasishaji wa vitendo vya ubakaji kwa kutumia dawa za aina hiyo. Wafuasi wake hawakumuonea haya walianza kumporomoshea mvua ya ‘diss’.

Mmwaka 2013, Rick Ross alijikuta akipoteza mchongo wa maana baada ya kuimba kwenye moja kati ya nyimbo alizoshirikishwa kuwa ‘alimuwekea dawa msichana kwenye kinywaji na kufanya naye mapenzi akiwa hajitambui’. Hali hii ilizua utata na alilazimika kuomba msamaha kwa kile alichodaiwa kuwa alikuwa anahamasisha ubakaji wa aina hiyo.

 

 

Njia rahisi za Kumgeuza Rafiki kuwa ‘Mpenzi Wako’ wa Dhati
NEC Yarudi, Yafafanua Kuhusu Idadi ya Wapiga Kura Kutofautiana Na Waliyotangaza