Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Nigeria, Peter Obi wa Peoples Democratic Party – PDP na Atiku Abubakar wa Chama cha Labour, wameandamana kupinga matokeo huku Obi akionesha nia ya kwenda Mahakamani kuwathibitisia Wanaigeria kuwa alishinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika februari 25, 2023.

Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria – INEC, wiki iliyopita, lilimtangaza Bola Tinubu wa chama tawala cha All Progressive Congress – APC, kama mshindi anayemrithi Rais Muhammadu Buhari anayemaliza muda wake kikatiba.

Katika uchaguzi huo, takriban watu milioni 25 walipiga kura katika kura kwa ya amani, lakini kulikuwepo na ucheleweshaji wa muda mrefu na hitilafu za kiufundi, hali iliyowakasirisha wengi wao na vyama vya upinzani ambavyo vimedai wizi wa kura ulifanyika.

Wafuasi wa Abubakar na wanachama wa PDP wakiwa wamevalia nguo nyeusi kuelekea makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi – INEC, jijini Abuja wakilalamikia udanganyifu katika uchaguzi.

Mwenyekiti wa PDP amesema “INEC inahusika moja kwa moja katika kusaidia wizi mkubwa na uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi kwa ajili ya chama tawala,” huku Kiongozi mwingine wa PDP Baraka Sani, akisema “kwa kweli ni hali ya kutisha, Okoa demokrasia yetu na INEC ni fisadi”.

Tume huru ya uchaguzi INEC, imekubali uwepo wa matatizo ya kiufundi siku ya kupiga kura lakini inakataa madai ya udanganyifu ambapo katika jitihada zake za kuboresha uwazi,mwaka huu ilianzisha utambulisho wa kibayometriki wa wapigakura kwa mara ya kwanza kitaifa.

Matatizo ya teknolojia mpya pia yalisababisha ucheleweshaji mkubwa na foleni, na kuwakatisha tamaa wapiga kura, huku huku wapiga kura waliojiandikisha wakiwa milioni 93.4, waliojitokeza kupiga kura walikuwa zaidi ya asilimia 27.

INEC, inatazamiwa kushughulikia baadhi ya maswala yaliyotolewa na vyama na wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa ugavana na mabaraza ya mitaa siku ya Jumamosi.

Wananchi wajiandikisha kupiga kura kwa ulinzi wa mtutu
Serikali kumlipa mshahara Adel Amrouche