Kungo kutoka nchini Rwanda na klabu ya Young Africans Haruna Niyonzima, amesema hana maneno mengi ya kuongea kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC, zaidi ya kuamini msema kweli ni dakika 90.

Young Africans itakuwa mgeni wa Simba SC Jumamosi (Mei 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha alama 57.

Niyonzima ambaye ni sehemu ya wachezaji wakongwe ndani ya Young Africans kwa sasa, amesema ana uzoefu wa kutosha na michezo inayowakutanisha dhidi ya Simba SC, na haamini kuwa timu yenye kiwango kizuri ndio ina nafasi kubwa ya kushinda kama inavyoelezwa na wadau wengi wa soka.

Amesema kwa kipindi chote alichocheza soka nchini Tanzania ameona maajabu mengi katika michezo inayozihusisha Simba SC na Young Africans, na kwa bahati nzuri amepata fursa ya kucheza kwenye timu hizo zenye maskani Kariakoo, jijini Dar es salaam.

“Hizi mechi zinakuwa ngumu, zinahitaji nidhamu na kuheshimu mpinzani wako, hata kama mmoja anakuwa kwenye ubora lakini ikifika wakati wa kukutana basi linakuwa sio jambo dogo, nani atashinda siku hiyo inategemea na upepo wa siku hiyo umevumia upande gani,” amesema Niyonzima.

Mpaka sasa Simba ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wamejikusanyia alama 61, wakifuatiwa na Young Africans wenye alama 57, licha ya kwamba wamecheza michezo miwili zaidi ya Simba.

Kortini kwa kuosha vipimo vya corona vilivyotumika
Saa chache kabla ya tamko la Facebook, Trump aanzisha tovuti yake