Naibu Katibu Mkuu wa Chama tawala nchini Burundi cha (CNDD-FDD) amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), katika uchaguzi uliofanyika Jijini Arusha.

Ntakarutimana amekuwa ni mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya wagombea wawili kutoka nchini Sudani Kusini, Gai Deng na Dk Anne Itto kujitoa dakika za mwisho na hivyo kusababisha mgombea huyo kukosa ushindani.

Joseph Ntakarutimana kutoka nchini Burundi (aliyenyanya bibilia) akiapa baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA).

Akisimamia uchaguzi huo, Katibu wa Bunge la EALA, Alex Obatre ametoa nafasi kwa wagombea hao waliojitoa kutamka kwa vinywa vyao kuwa wamejitoa, baada ya kuwasilisha taarifa rasmi ya kujitoa, ambapo wamesimama na kusema wana muunga mkono mpinzani wao.

Katika upigaji kura Spika huyo mpya amepata kura za ndiyo 54 kati ya kura 63 za wabunge  wote kutoka nchi saba za EAC, ambapo kura nane ziliharibika na kura moja haikupigwa kabisa.

Faru apewa jina la Waziri Mkuu
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 21, 2022