Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Joseph Omog ameamua kufungasha vilivyo vyake na kurudi nchini kwake Cameroon baada ya mkataba wake na klabu ya Simba kuvunjwa.

Omog alionekana uwanja wa ndege akiwa na mabegi saba yaliyoonekana kushiba vitu ndani yake kwani ndiyo anarudi moja kwa moja kwao.

Omog amesema anaondoka kwenda kwao, Cameroon kupumzika kwa mwezi mmoja, kisha ataangalia mustakabali wa wapi aende kufanya kazi.

“Nimemalizana na Simba kwa kila kitu ndiyo maana naondoka, siwezi kuzungumzia zaidi timu ya hapo kwa kuwa sipo tena ndani ya timu hiyo ila nawatakia kila la heri,” alisema Omog.

Mkata na klabu ya Simba ulivunjwa mara baada ya Simba kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho katika mchezo wake wa kwanza na timu ya Green Warriors ya Mwenge jijini Dar es Salaam kwa penati 4-3 baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Kwa sasa nafasi ya Simba inashikiliwa kwa muda na Kocha Msaidizi Masoud Djuma raia wa Burundi.

 

 

 

.

 

 

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 31, 2017
Mkaguzi ajinyonga kwa kipande cha chandarua