Mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England PFA, Gordon Taylor amemshauri na kumkingia kifua mshambuliaji wa klabu ya West Brom, Saido Berahino baada ya kuonyesha hasira kufuatia mpango wake wa kusajiliwa na klabu ya Tottenham Hotspurs kukwama.

Taylor ameamua kuchukua jukumu hilo kutokana na hali ya maelewano baina ya mshambuliaji huyo na viongozi wa klabu ya West Brom kuonekana kutokua shwari, ambapo imeelezwa kwamba Berahino anaamini viongozi wake hawakumtendea haki katika harakati zake za kujiunga na Spurs wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Berahino, alifikia hatua ya kuandika maneno mazito kuptia mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa kuwataka vuiongozi wake kuwa na mtazamo chanya katika mpango wake wa kusajiliwa na Spurs huku akiwaagiza kufanya maamuzi kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya jumanne.

Berahino mwenye umri wa miaka 22, alitoa agizo hilo kwa kutishia kugoma na kulazimisha uhamisho wake kukamilishwa ndani ya muda, hatua ambayo inakwenda kinyume wa taratibu za uweledi wa mchezaji ambaye ana mkataba katika ligi ya nchini England.

Kufuatia sakata hilo Tayler ameutaka uongozi wa West Brom kumsamehe mchezaji huyo na kuchukulia hatua aliyoichukua ya kuandika maneno makali kwenye mtandao wa kijamii kama sehemu ya hasira ambazo zilikua zimemjaa kwa kutaka jambo lake kufanikiwa.

Tayler pia ameutaka uongozi wa klabu ya West Brom kuwa na mpango mzuri wa kuwasikiliza wachezaji ambao ni wanachama wa PFA, pale linapojitokeza suala la klabu fulani kuonyesha nia ya kutaka kuwasajili.

Uhamisho wa Berahino kuelekea Spurs ulianza kuonekana hautokamilishwa wala kukubaliwa na viongozi wa The Baggies, baada ya ofa nne zilizotumwa na viongozi wa Spurs katika kipindi chote cha usajili ambacho kilifungwa rasmi siku ya jumanne saa kumi na mbili jioni kwa saa za nchini England.

Mwenyekiti wa West Brom Jeremy Peace anatajwa kuwa chanzo cha mambo yote yaliyotokea kwa kushirikiana na meneja wa kikosi cha The Baggies Tonny Pulis ambae walionyesha kutokua tayari kumuona Berahino akiondoka klabuni hapo.

Mke Wa Dk Slaa Amkana, Amwita Muongo
Magufuli: Mimi Ni Maji Moto Kuunguza Mafisadi