Shambulizi la kigaidi lililofanywa na kundi la Islamic States (IS) katika maeneo sita jijini Paris Ufaransa na kuua zaidi ya watu 127 usiku wa Ijumaa iliyopita yameumiza mioyo ya watu wengi.

Mwimbaji Justin Bieber jana alijikuta akimwaga machozi jukwaani wakati akitoa heshima zake kwa waathirika wa tukio hilo la kigaidi. Bieber alikuwa akitumbuiza jana usiku huko Los Angeles na kuanza kumwaga machozi wakati akiimba wimbo wa ‘I’ll Show You’.

Justin

Wakati sauti yake na sura yake vikionesha jinsi alivyokuwa katika dimbwi la majonzi akitoa machozi, Bieber alitoa maneno ya kufariji walioguswa na msiba huo huku maneno hayo yakimzidia, “We’re in this together.Why am I crying so hard?”aliuliza kabla hajaongeza “Get it together, Justin.”

Baada ya tamasha hilo, alipost picha yake akiwa analia na kuandika, “Tears are healthy”.

Wastara Atoa ya Moyoni Kuhusu Kukatwa Mguu Wake
Alichokisema Lowassa kuhusu Mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema Geita