Mwimbaji wa RnB, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo na mkewe aliyefunga naye ndoa hivi karibuni, Crystal Renay wameanza familia tayari.

Congrats to #NeYo & #CrystalRenay on the birth of their baby boy!

A photo posted by The Shade Room (@theshaderoominc) on


Wawili hao jana walipata mtoto wao wa kwanza wa kiume. Ingawa wawili hao hawajatoa tamko rasmi kufuatia baraka hiyo waliyoipata, picha ya mama na mwana iliyowekwa Instagram imeongea kwa sauti kubwa.

Renay ametumia mtandao wa Twitter kugusia kuwa huenda mtoto wao akaitwa ‘Shaffer Jr.’, akitohoa jina hilo kutoka kwa baba wa mtoto huyo.

Ugonjwa wa Kisukari Tishio nchini, Daktari Bingwa aeleza sababu ya ongezeko
Polisi na Takukuru wakunjana mashati kumgombea shahidi mahakamani