Mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ameanza kutimiza kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’ siku chache baada ya kuapishwa.

Profesa Jay ambaye ni rapa nguli, ameanza kazi ya kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara iliyo chini ya Halmashauri hiyo.

Amepost kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya picha zikimuonesha akiwa kazini na jumbe za kuwatia moyo wapiga kura wake.

Profesa Jay 2

“Wana MIKUMI Mmenikopesha KURA zenu Nitawalipa MAENDELEO!!” Profesa Jay aliandika Instagram.

Wananchi Kuamua Ukomo wa Urais wa Kagame Mwezi Huu
CUF wazungumzia taarifa za kufariki Maalim Seif, watoa msimamo wao kuhusu Uchaguzi Zanzibar