Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya upinzani kujikita katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na matamko ya uongo yanayo sababisha taharuki katika jamii na kuchonganisha wananchi na serikali yao.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo katika Ofisi ndogo Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Polepole amesema kuwa, wapinzani wamekuwa wakitumia matatizo ya wananchi kutoa matamko ya uongo ili kuitia nchi katika taharuki kwa lengo la kujitaftia umaarufu wa siasa, vitendo ambavyo havisaidii wananchi wala wanasiasa wa vyama hivyo katika kuleta maendeleo ya nchi.
“Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi, tuendelee kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo iliyoweka, ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda, hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka katika umasikini”, amesema Polepole.
Hata hivyo, Polepole amesema kuwa Tanzania haijawahi kupata  njaa yenye kiwango cha kuitwa baa la njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo wanaojaribu kutangaza kuwa nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa kufanya siasa safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM.

Video: Majaliwa afungua duka la dawa litakalo hudumia mikoa mitatu
Video: Mpinga apiga marufuku taa za mwanga mkali kwenye Magari