Mshambuliaji wa Chelsea Radamel Falcao ameumia tena na hataweza kucheza hadi katikati mwa Januari.

Falcao, 29, yumo Chelsea kwa mkopo kutoka Monaco lakini hajaweza kuchezea Blues tangu mechi dhidi ya Liverpool 31 Oktoba, ambayo walichapwa 3-1.

Kaimu meneja wa Chelsea Guus Hiddink anasema tatizo la misuli ya paja limejirudia Falcao akiwa mazoezini, na itamchukua hadi “siku 10” kuweza kucheza tena.

“Tunarudi tena tulikoanzia,” mholanzi huyo amesema. “Tulimshirikisha mchezaji na akapata jeraha hili. Tunatumai atakuwa sawa tena baada ya siku 10, ingawa hataweza kuchezeshwa wakati huo.”

Falcao, alikaa msimu uliopita kwa mkopo Manchester United.

Hayo yakijiri, Hiddink ameeleza kusikitishwa kwake na tangazo la meneja wa Aston Villa Remi Garde kwamba anamtaka Loic Remy.

“Lazima uheshimu wachezaji walio katika klabu nyingine,” amesema Hiddink.

“Iwapo unataka mchezaji, zungumza kwanza na klabu ambayo anachezea. Huwezi kutangaza hadharani.”

Remy amekuwa akitatizwa na majeraha, kwa mujibu wa Hiddink, na lazima kwamba athibitishe kwamba yeye ni mchezaji mzuri.

 

Kagame atoa tangazo rasmi la Utawala wa Muhula wa Tatu
Danny Welbeck Atuma Salamu Za Mwaka 2016 Afrika