Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametangaza rasmi kuwa atawania urais wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu baada ya muhula wa pili kukamilika mwaka 2017.

Rais Kagame ametoa tangazo hilo likiwa katikati ya salamu za kuwatakia wananchi wake heri ya mwaka mpya 2016 alilolitoa leo.

“Mmeniomba niongoze nchi hadi baada ya mwaka 2017. Kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili kwenu, sina budi kukubali,” alisema Kagame kwenye salaam zake.

Hata hivyo, Kagame ambaye asilimia 98 ya wananchi wa Rwanda walimuidhinisha kugombea tena muhula wa tatu, alisema kuwa hataiongoza nchi hiyo hadi kufa kwake.

 

Hoteli za Double Tree, Slipway na Nyumba ya Kigogo Huyu Vyasombwa na 'Bomoabomoa'
Radamel Falcao Yu Hoi Bin Taaban