Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewapa neema ya ajira vijana zaidi ya 2000 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki shughuli mbalimbali za ujenzi za Serikali.

Walioneemeka na tangazo la ajira la Rais Magufuli ni wale walioshiriki ujenzi wa Ukuta wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, nyumba za magereza na wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Malale kwa kujitolea.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mji wa Serikali, Ihumwa jijini Dodoma, Rais Magufuli alielekeza vijana hao wapewe ajira katika maeneo mbalimbali ya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Idara ya Uhamiaji, Idara ya Usalama wa Taifa, Takukuru, Jeshini na taasisi nyingine za kiserikali.

Awali Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo alimuomba Rais kutoa neno moja ambalo litawapa faraja vijana hao waliojitolea kufanya kazi muhimu za kujenga nchi.

Rais Magufuli amempandisha cheo kiongozi wa kazi hizo za ujenzi, Kanali Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 14, 2019
Manny Pacquiao aanza kumpika mwanaye, mkewe atokwa machozi

Comments

comments