Juhudi za Ray C kutaka kurudi kama zamani zimezaa matunda kwa kuanza na mwili wake ambao miaka ile uliwafanya wanaume watafutane kila alipopanda jukwaani na kuzungusha kiuno kama ‘feni mpya’.

Mrembo huyo ambaye amefanikiwa kuachana na madawa ya kulevya huku akiimalizia kuiweka sawa albam yake mpya, amesema kuwa amefanikisha ndoto yake ya kupunguza uzito kilo 30 na kurudi kama zamani.

Ray C amepost Instagram maelezo na picha inayoonesha dhahiri kuwa ‘Kiuno Bila Mfupa’ kimerudi.

50 Cent Aonesha Mjengo Wake Mpya Wa Kifahari Ulioko Afrika
Kim Kardashian Azungumzia Taarifa Za Kukuchukua Video Wakati Akijifungua