Ripoti ya Kamati mbili zilizoundwa na Bunge kuchunguza biasahara ya madini aina ya Tanzanite na Almas zilizowasilishwa kwa Spika, Job Ndugai zimeitaka Serikali kuwachukulia hatua mawaziri wote waliohusishwa na biashara hiyo.

Mawaziri hao wa zamani waliotajwa katika ripoti hiyo ni Prof. Sospeter Muhongo, William Ngeleja na George Simbachawene wanaodaiwa kufanya makosa ya kiutendaji walipokuwa wakiongoza wizara hiyo.

Aidha, Kamati hiyo pia imeitaka Serikali kuwachukulia hatua maofisa wa zamani wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) akiwemo Mhandisi Edwin Ngonyani ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wajumbe wa Shirika hilo pamoja na mkurugenzi wa kuthaminisha madini.

Hata hivyo,  Kamati hiyo imependekeza kufanyika kwa uhakiki wa gharama za uwekezaji kuanzia mwaka 1994 hadi sasa, wajumbe wa bodi wawajibishwe, ufanyike uchunguzi katika wa mitambo ya migodi pia walihusika na mikataba hiyo mibovu wachukuliwe hatua stahiki.

 

LIVE IKULU: Rais Magufuli akipokea ripoti ya uchunguzi wa Tanzanite na Almasi
Kim kardashian kuongeza mtoto wa tatu kwa gharama kubwa