Jaji Mkuu wa shindano la Bongo Star Search na Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark production, Ritha Paulsen rasmi amezindua msimu mpya wa kumsaka kipaji wa kuimba kupitia kipindi chao ambapo amesema katika msimu huu wa 10 Jaji Salama Jabir hatoweza kushiriki kama miongoni mwa majaji kama ambavyo imekuwa misimu iliyopita.

Akizungumza Master J ambaye pia ni jaji wa shindano hilo amesema kuwa watamkumbuka sana Salama na walitamani awepo lakini majukumu ya kikazi yameingiliana hivyo hatoweza kushiriki.

”Nasikitika zaidi kwamba mwaka wa 10 tunafanya msimu bila yeye ni basi tu kwamba amepata mkataba ‘contract’ ambazo kidogo ratiba zinagongana na ratiba yetu ya BSS mwaka huu tutammiss sana , lakini hao ambao wamechaguliwa Jide na Dully ni watu ambao tayari nina chemsitry nao tena miaka ishirini, watu mkishakuwa na chemistry nzuri judges ata content inakuwa nzuri”. Amesema Master J.

Mbali na kutokuwepo kwa Salama Jabir yapo mabadiliko mengine makubwa ambayo yamefanyika upande wa majaji na watangazaji ambapo msanii Lady Jay Dee binti komando na Dully Skyes wataungana na Master J na Ritha Paulsen kwenye kujaji washiriki katika shindano hilo, huku Idris Sultan kushikilia nafasi ya Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Siza Daniel ambao msimu uliopita walikuwa mtangazaji.

Bongo Star Search msimu huu wa 10 inatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza Septemba 28 na 29, mkoani Arusha.

Aidha madam Ritha katika uzinduzi huo amesema kuwa zipo changamoto nyingi ambazo anakumbana nazo katika uandaaji wa shindano hilo lakini amekuwa mstari wa mbele kukabiliana nazo na kuhakikisha lengo la kuwainua na kuwatambua vijana walio mtaani na wenye vipaji wanafanikiwa na wanafika mahali fulani.

Wapo wasanii ambao wametokea mlango wa Bongo Star Search akiwemo Peter Msechu, Kala Jeremiah, Walter Chilambo, na wengine wengi.

 

Alikiba - Ni kweli mke wangu nilimrudisha kwao, wasipende kuingilia maisha ya watu
Tanzania yapanda kwenye viwango vya FIFA