Mtunzi mahiri wa nyimbo na muimbaji, Barnaba amepanga kuigusa tasnia ya nyimbo za injili kwa kufanya nyimbo nne za upako.

Barnaba ameeleza kuwa anapenda sana nyimbo za injili na kwamba muda wowote anaweza kuachia nyimbo hizo nne na yuko tayari hata kuzungumza kwenye matamasha ya injili.

“Napenda sana gospel na kuna nyimbo zinakuja na kama ikitokea show nitafanya,” Barnaba alikiambia kipindi cha Chomoza cha Clouds TV.

barnaba (1)

Hata hivyo, Barnaba ataendelea kuwa mwimbaji wa Bongo Flava anaegusa pia nyimbo za injili.

Kipyenga Cha Ligi Kuu Kupulizwa J.Mosi
Inler: Tukitanguliza Furaha Ya Kufuzu Itakula Kwetu