Serikali imesema kuwa imeunganisha Taasisi 72 katika mtandao wa Mawasiliano Serikalini kupitia mkongo wa Taifa, na kufikia Desemba Taasisi zingine 77  zilizopo chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora zitakuwa  zimeshaunganishwa, ambapo kukamilika kwa  miundo mbinu hiyo kutaipunguzia Serikali gharama za uendeshaji wa mawasiliano zilizokuwa  zinatolewa.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wakala wa Serikali Mtandao, Suzani Mshakangoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa Serikali itaboresha utoaji utoaji huduma kwa Umma kwa kusaidia Taasisi kuwa na mawasiliano bora ya kielektroniki masafa ya inteneti.

Amesema Taasisi zilizo unganishwa na mfumo huo wa simu za inteneti zitaweza kuwasiliana na Taasisi zingine kwa urahisi na zitaweza kufanya mikutano na washiriki mbali mbali kwa njia ya simu (teleconference) ili kufanikisha lengo lao.

Aidha, Mshakangoto amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wakala imetoa mafunzo kwa taasisi ili kuweza kurahisisha matumizi ya simu zinazo tumia itifaki (IP Phones) kwa wataalamu wa TEHAMA na makatibu muhtasi kutoka kwa wizara na taasisi zinazojitegemea.

Hata hivyo amesema kuwa Serikali ina mpango wa kuifikia Mikoa na Halmashauli zote nchini ili kutumia mawasiliano ya simu  za itifaki, barua pepe na mifumo ya TEHAMA katika kubadilishana taarifa.

Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2012 kwa  sheria ya Wakala za Serikali Na.30, sura ya 245 ya mwaka 1997 ya kuratibu  na kusimamia  Serikali  Mtandao nchini.

 

Ray C aingia ‘jikoni’ na Damian Soul
Audio: Taarifa ya Polisi Tanga kuhusu kukamatwa majambazi waliovamia chuo kukuu.