Mkurugenzi wa ufundi wa zamani wa Ferrari Chase Carey ambaye alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya mshauri wa Liberty ameteuliwa kuongoza kazi za ufundi katika kampuni ya mashindano ya Formula One kuchukua nafasi ya Bernie Ecclestone.

Bernie ameondolewa katika nafasi yake ya kudhibiti mashindano ya magari ya langalanga ya formula one baada ya shirika la habari la Liberty la Marekani kukamilisha mkataba wake wa dola bilioni 8 ya kumiliki mchezo huo. Liberty pia imemnunua meneja wa zamani wa magari ya Mercedes, Ross Brawn kwa mashindano ya Formula 1.

Liberty ilianza kutaka kumiliki mashindano hayo ya magari ya langalanga mwezi Septemba mwaka jana, na mapema Januari mwaka huu walikamilisha masharti mawili ya kisheria yaliokuwa yamesalia. Mpango huo ulikamilika siku ya Jumatatu na shirika la habari la Liberty linatarajiwa kubadilisha jina lake na kutumia jina la kundi la Formula

UVCCM yautabiria mabaya upinzani
Ivory Coast Yavuliwa Ubingwa AFCON 2017