Beki kutoka nchini Ujerumani Shkodran Mustafi ameachwa kwenye kikosi cha klabu ya Valencia kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha wachezaji kutoka nchini Nigeria (Nigeria All-Stars) baadae hii leo.

Meneja wa klabu ya Valencia Pako Ayestarán, amefanya maamuzi ya kumuweka pembeni beki huyo bila kutoa ufafanuzi wowote, japo imeanza kuhisiwa huenda mipango ya Mustafi kuondoka ikawa imekaribia kutokana na fununu za kuwa mbioni kujiunga na Arsenal.

The Gunners, wamekua katika hatua za kutaka kusajili mchezaji anaecheza nafasi ya ulinzi kutokana na tatizo linalowakabili hivi sasa, la kuwakosa mabaki wao Per Mertesacker na Gabriel ambao ni majeruhi huku Laurent Koscielny akiwa bado hajapata mazoezi ya kutosha ya kurejea katika kikosi cha kwanza, baada ya kutoka mapumziko kufuatia jukumu lililokua likimkabili la kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa wakati wa fainali za Euro 2016.

Hata hivyo Calum Chambers na Rob Holding wameendelea kuwa kikosini na wanatumika kama chaguo la kwanza la Arsene Wenger katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini England pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mustafi amekua katika chaguo la kwanza la meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kuaminiwa huenda akawa jibu la kutatua tatizo la ulinzi ambalo linaonekana kuwa changamoto kubwa kuelekea katika mchezo wa ufunguzi wa msimu, ambapo The Gunners watapambana na Liverpool katika uwanja wa Emirates mwishoni mwa juma hili.

Wakati Arsenal wakipanga mikakati ya usajili wa Mustafi, Valencia wamejizatiti kumuhamisha beki wa Manchester City, Eliaquim Mangala kama mbadala wake.

Kikosi cha wachezaji 23 cha Valencia kilichotajwa tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya wachezaji kutoka nchini Nigeria (Nigeria All-Stars) upande wa makipa ni Diego Alves, Ryan na Jaume Doménech.

Mabeki: Cancelo, Montoya, Vezo, Santos, Abdennour, Orban, Gayà na Lato.

Viungo: Enzo Pérez, Parejo, Róber, Nani, Carlos Soler, Fede Cartabia, Rafa Mir,Santi Mina, Medrán na Bakkali.

Washambuliaji: Rodrigo, Paco na Alcácer.

Nyambizi Ya Manjano Yapata Pigo, Majibu Kutoa Mustabali
Naibu Waziri Mpina Aiasa Taasisi Ya Muungano Kufanya Tafiti Zenye Tija Kwa Serikali Na Umma