Mabingwa watetezi Tanzania Bara Simba SC, wameendeelea kujikita kileleni baada ya kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-0.

Mashabiki waliokua wakiufuatilia mchezo huo uliounguruma kwenye Uwanja wa CCM Krumba jijini Mwanza, walishudia Simba SC wakipata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha na mshambuliaji wao John Bocco dakika ya 17.

Mshambuliaji kutoka DR Congo Criss Mugalu aliipatia Simba SC bao la pili dakika ya 62, huku Bocco akifunga bao la tatu dakika ya 86.

Simba sasa imefikisha alama 67 , ikicheza michezo 27, ikifuatiwa na Young Africans yenye alama 61 zilizopatikana kwenye michezo 29.

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 60.

Wakati huo huo John Bocco amfikisha mabao 13 msimu huu kwenye ligi kuu na goli la 7 kwenye michezo 4 ya mwusho aliocheza.

Basata wampongeza Diamond kuwania Tuzo ya BET 2021
Ndugulile ataka wasiolipa kodi waondolewe